1xbet

BREAKING!! SPAIN YATIMUA KOCHA SIKU MOJA KADBA YA KUANZA MICHUANO KOMBE LA DUNIA!!!

Breaking: Taarifa zaidi zilizojitokeza zinasema kwamba Rais wa shirikisho la soka la Spain Luis Rubiales amekasirishwa sana na kitendo cha Julen Lupetegui na Real Madrid kutangaza kuwa kocha huyo atajiunga na mabingwa hao wa ulaya siku 2 kabla ya World Cup. Akieleza kitendo hicho sio cha kiungwana kwasababu Lupetegui alisaini mkataba mpya na Spain siku 21 zilizopita, lakini pia inaelezwa jambo hilo limeleta mgawanyiko ndani ya kikosi ambacho kimesheheni wachezaji wa vilabu pinzani vya Uhispania Atletico, Barca na Real Madrid - ikielezwa Lupetegui anaweza kutumia nafasi ya kukaa karibu na wachezaji ambao baadae anaweza kutaka kuwasajili akiwa katika ajira yake mpya na Los Blancos. 
:
Mpaka sasa inaelezwa Fernando Hierro na kocha wa timu ya vijana ya Spain U21 Albert Celades - huenda hawa wakapewa fursa ya kuliongoza jahazi la Spain katika michuano hii Ikiwa Lupetegui atafukuzwa kazi muda mfupi ujao!